DAWA GANI ITAMSAIDIA MTOTO KUPATA CHOO(tatizo la mtoto kukosa choo)

 AFYA KWA MTOTO

• • • • • •

DAWA GANI ITAMSAIDIA MTOTO KUPATA CHOO(tatizo la mtoto kukosa choo)


Baada ya  mtoto kuzaliwa huanza kunyonya maziwa ya mama yake, na baada ya muda huanza kujisaidia haja ndogo na haja kubwa pia. Lakini kukaa kwa muda mrefu bila mtoto kupata choo huweza kuleta mashaka hata kwa mama wa mtoto pia.


Swala la mtoto kukosa choo kwa muda mrefu huweza kusababisha mtoto kulia lia mara kwa mara, Mtoto kupata maumivu ya tumbo,tumbo kujaa n.k


Wengine tatizo la kukosa choo kabsa, huanza na haja kubwa kuwa ngumu sana wakati wa kujisaidia, Kujisaidia kinyesi kama cha mbuzi na baadae hali ya kukosa choo kabsa hujitokeza.


Watoto wadogo sana huweza kupatwa na shida hii, Watoto ambao ni kuanzia mwaka mmoja mpaka miaka mitano pia huweza kusumbuliwa na shida hii.


DAWA GANI ITAMSAIDIA MTOTO KUPATA CHOO(tatizo la mtoto kukosa choo)


- Zipo njia mbali mbali ambazo hutumika kutatua tatizo hili kulingana na Umri wa mtoto, Mfano;

Kwa watoto ambao tayari wanakula vyakula vingine tofauti na maziwa ya mama pekee, hushauriwa ;

• kula matunda ambayo yana nyuzi nyuzi kama maembe,machungwa na matunda yenye kiwango kikubwa cha maji kama matikiti maji,

• Watoto kunywa kiwango kikubwa cha maji kwa siku

• Watoto kuepuka kubana kinyesi kila mara wanapohisi haja kubwa

• Lakini pia kuna njia ya kumassage tumbo la mtoto, hali ambayo itamsaidia mtoto kujisaidia kwa haraka zaidi.


Lakini pia unaweza kuonana na wataalam wa afya hasa wa mambo ya Watoto kwa ajili ya Msaada zaidi.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!