BAKTERIA
• • • • •
FAHAMU FAIDA ZA BAKTERIA MWILINI(sio kila bakteria wana madhara)
Bila shaka hata wewe unayesoma na kufwatilia makala hii ukisikia neno bakteria moja kwa moja unafikiri kwamba wanaleta magonjwa makubwa.
Kuna vimelea vingi kama vile; Fangasi, Virusi,Protozoa na jamii hii ya Bakteria ambavyo huweza kusababisha magonjwa mbali mbali kwenye mwili wa binadamu.
Lakini pia kuna bakteria ambao ni wema na hufanya kazi kubwa ya kusaidia mwili wako, endapo bakteria hawa wasingekuwepo huenda ungeumwa vilevile.
FAIDA ZA BAKTERIA WEMA MWILINI NI PAMOJA NA;
- Kusaidia kuleta hali ya usawa na kukukinga na baadhi ya vimelea vingine vya magonjwa nyemelezi
- Baadhi ya bakteria husaidia sana katika swala nzima la umeng'enyaji wa chakula mwilini
- Baadhi ya bakteria husaidia sana katika uzalishaji wa vitamins Kama vile; Vitamin B6 Na Vitamin B12.
- Baadhi ya bakteria husaidia katika ulainishaji wa chakula unachokula
N.K
Hivo basi, Fahamu kwamba sio kila bakteria ni mbaya, Wengine wanaumuhimu wake wakiwa katika kiwango kinachotakiwa mwilini
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!