NGOZI
• • • • • •
FAHAMU KUHUSU KUPANDIKIZA NGOZI kwa kitaalam Skin grafting
Ngozi hufanya kazi nyingi sana katika mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na kuwa kama kinga ya kuzuia vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile Bacteria kuingia ndani kwenye mwili wako.
SKIN GRAFTING ni maneno ya kingereza au kitaalam yakiwa na maana ya kitendo cha kutoa ngozi sehemu moja ya mwili na kuiweka sehemu nyingine ya mwili,kutoka kwa binadamu mmoja kwenda kwa mwingine au kutoka kwa viumbe vingine kama samaki kwenda kwa binadamu.
Kitendo hiki cha kupandikiza ngozi huweza kufanyika kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, Sehemu moja kwenda nyingine au hata kutoka kwa kiumbe kimoja kwenda kwa binadamu,Mfano kama vile kutoka kwa Samaki kwenda kwa binadamu kama kwenye picha hapo chini.
Mtu huweza kupandikizwa ngozi kutokana na sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na sababu au ajali ya Kuungua kwa moto au sababu nyingine yoyote ambayo huhusisha sehemu kubwa ya ngozi kuharibika sana au kuondoka.
Upandikizwaji wa ngozi huweza kufanyika katika maeno mbali mbali ya mwili kama vile; Miguuni,mikononi,kwenye makalio N.K
Au hata mwili mzima mtu huweza kufanyiwa Skin Grafting.
(Picha; Mtoto mdogo akifanyiwa skin grafting kwa kutumia Ngozi ya Samaki)
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!