HOSPITAL
• • • • •
FAIDA ZA MHUDUMU WA AFYA KUMSHIRIKISHA MGONJWA KWENYE TIBA
Ukweli ni kwamba ili tupate tiba sahihi na Mgonjwa kupona lazima kuwe na ushirikiano mzuri kati ya Mtoa huduma pamoja na Mgonjwa wake.
Moja ya msingi imara katika kuanza tiba ni pamoja na Mgonjwa kujielezea vizuri kuhusu tatizo lake ambalo kwa kitaalam kitendo hiki tunaita Patient History Taking.
Tiba sahihi huanza na maelezo sahihi kutoka kwa Mgonjwa, Na Maelezo sahihi kutoka kwa Mgonjwa hutegemea na ushirikiano Mzuri kutoka kwa mtoa huduma wake ikiwa ni pamoja na Lugha yake,ukarimu wake N.K.
Hivo watu hawa wawili huwezi kuwatenganisha katika kutatua tatizo la Mgonjwa.
Ni lazima Mtoa huduma wa afya kumshirikisha Mgonjwa wake katika kila hatua ya tiba ambayo anaifanya, ikiwa ni pamoja na vipimo anavyochukua kwa Mgonjwa na kumpa maelekezo ya kina kwanini anachukua vipimo hivo, Na hata baada ya majibu kutoka lazima amuelezee mgonjwa wake kwa kina kuhusu majibu yake.
Lakini pia ni jukumu lako kuuliza pale ambapo hupati majibu yanayoeleweka ili ujue tatizo gani hasa linausibu mwili wako na matibabu yake ni yapi.
FAIDA ZA MHUDUMU WA AFYA KUMSHIRIKISHA MGONJWA KWENYE TIBA
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!