KAMBA
• • • • • •
FAIDA ZA ZOEZI LA KURUKA KAMBA
Moja ya vitu muhimu sana katika kuimarisha afya ya mwili ni pamoja na kufanya mazoezi, Ukishindwa sana tenda angalau dakika 30 kila siku za kufanya mazoezi.
Kuna aina nyingi sana za mazoezi kama vile; mazoezi ya jim, Kunyanyua vitu vizito, kuruka kamba, zoezi la kukimbia, zoezi la kucheza mpira(mpira wa miguu,mpira wa kikapu N.K)
BAADHI YA FAIDA ZA MAZOEZI MBALI MBALI KWA UJUMLA WAKE NI PAMOJA NA;
- Kuimarisha kinga ya mwili wako
- Kuleta afya ya ngozi
- Kupunguza uwezekano wa kushambuliwa na magonjwa mbali mbali kama vile magonjwa ya moyo,Kisukari,Presha N.K
- Kupunguza uzito wa mwili na kukusaidia kuondokana na shida ya kuwa na uzito uliopitiliza
N.K
FAIDA ZA ZOEZI LA KURUKA KAMBA KWA UPEKEE WAKE
Faida za zoezi la kuruka kamba ni pamoja na;
• Kusaidia kupunguza presha au shinikizo la damu kwa watu wenye shida hii
• Kuruka kamba husaidia sana katika kuchoma mafuta mabaya mwilini
• Kuruka kamba husaidia sana katika kuimarisha afya na kuukinga moyo dhidi ya magonjwa mbali mbali
• Kuruka kamba husaidia kuimarisha mzunguko mzuri wa hewa mwilini ikiwa ni pamoja na kutanua mapafu vizuri
• Kuruka kamba husaidia sana kupunguza uzito wa mwili kwa watu wenye tatizo la uzito mkubwa
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!