FANGASI
• • • • • •
FANGASI WA KUCHA(chanzo,dalili,tiba)
Kuna aina nyingi za fangasi kama vile; Fangasi wa kucha, fangasi wa koo, Fangasi wa damu,fangasi wa ulimi,fangasi wa mdomoni,fangasi sehemu za siri N.K
Lakini katika makaa hii tunazungumzia kuhusu fangasi wa kucha.
Watu wengi hupata shida hii ya mashambulizi ya fangasi wa kucha, huku baadhi yao wakipona bila hata matibabu,lakini endapo fangasi hawa wamefikia hatua ya kukusababishia maumivu sana ya kucha,kucha kivimba,kucha kuoza N.K lazima upate tiba.
Fangasi wa kucha huweza kusababisha;
- kucha kuoza
- kucha kutoa harufu mbaya
- maumivu ya kucha
- kucha kuvimba
- kucha kupoteza kabsa shape yake
WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA FANGASI WA KUCHA
✓ Watu wenye historia ya fangasi wa miguuni,vidoleni N.k
✓ Wazee( kutokana na kupungua kwa mzunguko wa damu maeneo ya kucha hivo kupelekea urahisi wa mashambulizi ya fangasi kuchani)
✓ Watu ambao hupenda kutembea peku
✓ Watu ambao huvuja jasho sana miguuni au mikononi
✓ Watu wenye tatizo la kisukari
✓ Watu ambao wameumia kwenye kucha
MATIBABU YA FANGASI WA KUCHA
Kutibu fangasi wa kucha huweza kuhusisha matumizi ya dawa mbali mbali za fangasi kama vile; itraconazole
Hivo kutana na wataalam wa afya upate matibabu juu ya tatizo lako.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!