KUMBIKUMBI
• • • • •
JE ULAJI WA KUMBIKUMBI UNA MADHARA GANI MWILINI?
Kumbikumbi ni aina flani ya wadudu ambao hupatikana kwenye maeneo mbali mbali na katika misimu flani ya hali ya hewa, Mfano kipindi cha Mvua N.k
Wadudu hawa wa kumbikumbi huitwa majina mbali mbali kulingana na Jamii flani na tamaduni za jamii hiyo,
huku baadhi ya watu wakila wadudu hao na wengine kutotaka hata kuwaona kabsa.
Baadhi ya jamii huamini kumbikumbi wana madhara mwilini, Wakati jamii zingine huamini kwamba kumbikumbi wanafaida nyingi mwilini ikiwa ni pamoja na imani kuwa ni dawa ya baadhi ya magonjwa kama maumivu ya mgongo N.K.
JE KUMBIKUMBI WANA MADHARA UKILA?
Ukweli ni kwamba wadudu hawa wa kumbikumbi hawana madhara yoyote mwilini badala yake wadudu hawa wanaweza kuwa ni faida pia.
Kumbikumbi huweza kusaidia kuongeza kiwango cha protein mwilini mwako japo kwa asilimia chache ukilinganisha na vyakula vingine kama nyama,samaki maharage N.K
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!