JINSI YA KUFANYA MAZOEZI YA KUTEMBEA ILI KUPUNGUZA TUMBO

 AFYA TIPS

• • • •

JINSI YA KUFANYA MAZOEZI YA KUTEMBEA ILI KUPUNGUZA TUMBO


Watu wengi hawafahamu kwamba mazoezi ya kutembea ni mazoezi mazuri sana katika kupunguza mafuta ya mwili,unene,uzito kupita kiasi pamoja na wanawake wenye changamoto ya tumbo kubwa.


Chamsingi lazima ufahamu jinsi ya kufanya mazoezi haya ili kufikia malengo yako.


JINSI YA KUFANYA MAZOEZI YA KUTEMBEA ILI KUPUNGUZA TUMBO


Ukweli ni kwamba ili kupunguza uzito,mwili wako unahitaji kuchoma kiwango kikubwa cha mafuta mwilini kuliko kile inachotumia.


Kufanya mazoezi ya kutembea husaidia sana kuunguza kiwango cha mafuta mwilini,


- Tafiti zinaonyesha kwamba, kutembea umbali wa Wastani wa Kilomita 1.6 husaidia kuunguza kiwango cha mafuta Calories 100 mwilini kwa kutegemea uzito ulio nao pamoja na Jinsia yako.


- Tafiti nyingine ikaonyesha kwamba, Mwanamke ambaye hutembea kwa dakika 50 mpaka 70 mara tatu kwa wiki nzima ndani ya wiki 12, inapunguza mafuta yako ya mwili kwa kiwango cha asilimia 1.5%.


Hivo anza leo kufanya mazoezi ya kutembea  kwa ajili ya afya yako.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!