MAGONJWA YA ZINAA
• • • • • •
JINSI YA KUJIKINGA NA MAGONJWA YA ZINAA
Kwa utangulizi, Magonjwa ya Zinaa ni magonjwa ambayo huenezwa kwa njia ya kujamiiana au kufanya mapenzi(Ngono).
Miongoni mwa magonjwa ya zinaa ni pamoja na kaswende au kwa kitaalam hujulikana kama Syphilis,kisonono au wengine husema GONO ikiwa na maana ya kifupi cha neno Gonnorhea,Chlamydia na Ukimwi.
JINSI YA KUJIKINGA NA MAGONJWA YA ZINAA
1. Epuka tabia ya kuwa na wapenzi wengi, kuwa na mtu mmoja au wengine wanasema baki njia kuu.
Hii itakusaidia sana kukuepusha na hatari ya kupatwa na magonjwa mbali mbali ya zinaa.
2. Epuka ngono zembe, Tumia kinga au Condom wakati wa kujamiiana.
3.Epuka matumizi ya pombe kupita kiasi. Moja ya tabia ambayo huhusishwa na ngono zembe pamoja na kupata magonjwa mbali mbali ya zinaa ikiwa ni pamoja na ukimwi,
ni matumizi ya pombe kupita kiasi, tabia ambayo humfanya mtu ashindwe kujidhibithi mwenyewe.
4. Epuka tabia ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile.
5. Epuka matumizi ya madawa ya kulevyia ikiwa ni pamoja na sindano za kujidunga, kwani tafiti zinaonyesha watu wengi ambao ni waraibu wa madawa haya ya kulevyia pia hupata maambukizi ya virusi vya ukimwi.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!