Ticker

6/recent/ticker-posts

JINSI YA KUWA NA MENO YENYE AFYA BORA(afya tips)



 AFYA TIPS

• • • • 

JINSI YA KUWA NA MENO YENYE AFYA BORA(afya tips)


Kuna mambo mbali mbali ya kuzingatia kwa ajili ya ulizi wa meno yako, hakikisha unasoma makala hii mpaka mwisho. 


KUMBUKA; watu wengi kwa hivi sasa wanasumbuliwa na matatizo ya meno, ikiwa ni pamoja na meno kuuma sana, meno kubadilika rangi, meno kutoboka N.k


JINSI YA KUWA NA MENO YENYE AFYA BORA(afya tips)


1. Hakikisha unasafisha meno baada ya kula chakula na kuacha meno yakiwa hayana mabaki yoyote ya chakula.


Unashauriwa angalau utumie dakika mbili kusafisha meno yako kwa kutumia mswaki na dawa ambayo ina Fluoride,ili kusaidia kuondoa uchafu na vimelea vya magonjwa kama bacteria.


2. Ulaji wa chakula bora yaani balance diet sio faida kwa mwili tu ni pamoja na kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa,afya ya meno pamoja na Fizi.


3. Ukishindwa kusafisha meno yako kila baada ya kula,jitahidi angalau kusafisha meno mara mbili kwa Siku.


4.Ulaji wa vyakula vigumu sana au vyakula vyenye mawe au mchanga huweza kusababisha ubovu wa kudumu wa meno yako.


MAMBO YA KUEPUKA KWA AJILI YA KUTUNZA MENO YAKO


- Epuka kulala bila kupiga mswaki baada ya kula chakula,kwani utalala na mabaki ya chakula na kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya bacteria kuzaliana


- Epuka kula vyakula vigumu,vyenye mchanga au mawe mara kwa mara


- Epuka kusafisha meno yako kwa vitu kama sabuni, mkaa N.k Tumia dawa za meno zenye fluoride ndani yake


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments