JINSI YA KUZUIA UTI KWA WATOTO WA KIKE

UTI

• • • • • •

JINSI YA KUZUIA UTI KWA WATOTO WA KIKE


Kama ilivyo kwa mtu mzima wa jinsia ya kike vivyo hivyo hata kwa mtoto mdogo wa kike huweza kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa uti kuliko mtoto wa kiume.


Hivo basi, kwa mzazi au Mlezi kuna mambo mbali mbali ya kuzingatia ili mtoto wako asiwe na tatizo la UTI za mara kwa mara.


MAMBO YA KUZINGATIA KWA MTOTO WA KIKE ILI KUMKINGA NA UTI


1. Wakati wa kumsafisha mtoto baada ya kujisaidia, hakikisha unamsafisha mtoto kutoka mbele kurudi nyuma(sehemu ya haja kubwa).


Hii itaepusha kutoa uchafu kutoka sehemu ya haja kubwa kuingiza sehemu za siri za mtoto, kwani kumsafisha mtoto kutoka nyuma kwenda mbele, unaweza kuhamisha uchafu wa haja kubwa pamoja na vimelea vya magonjwa na kuviingiza sehemu ya haja ndogo. Kitu ambacho huweza kusababisha mtoto kuwa na maambukizi ya UTI.


2. Pia tafiti zinaonyesha kwamba endapo mtoto amekaa na kinyesi kwenye pampasi kwa muda mrefu, huweza kuwa rahisi uchafu(kinyesi) pamoja na vimelea vya magonjwa kuingia kwenye njia ya haja ndogo na Kuleta ugonjwa wa UTI kwa mtoto.


Hivo epuka tabia ya kumuacha mtoto na pampasi kwa muda mrefu baada ya mtoto kujisaidia.


.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!