KANSA KATIKA NJIA YA HAJA KUBWA(dalili,tiba)

 KANSA

• • • • •

KANSA KATIKA NJIA YA HAJA KUBWA(dalili,tiba)


Hii ni aina ya kansa ambayo ni mara chache sana kutokea pengine hata wewe ukashangaa hivi kumbe kuna kansa ya njia ya haja kubwa, ila ukweli ipo.


CHANZO CHA KANSA HII


- kansa hii husababishwa na kirusi kinachojulikana kwa jina la Human papilloma virus au HPV kwa kifupi, na watu ambao wapo kwenye hatari ya kupata ni pamoja na;


1. Wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile yaani Anal Sex


2. Watu wenye wapenzi wengi


3. Wavutaji wa sigara


4. Wenye kansa ya ukeni au kansa ya shingo ya kizazi


5. Wanaofanya mapenzi bila kinga


6. Wenye shida ya kinga ya mwili kuwa ndogo


7. Wale wanaoshare Sex toys


8. Wenye magonjwa kama Ukimwi N.k


DALILI ZA KANSA HII


Kansa hii hutokea mara chache sana, japo inaweza kutokea na kwa kitaalam hujulikana kama Anal cancer,na baada ya kutokea mgonjwa huweza kupata dalili mbali mbali kama vile;


- Kutokwa na usaha njia ya haja kubwa


- Kutokwa na damu au kinyesi kilichochanganyika na damu sehemu ya haja kubwa


- Kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia haja kubwa


- Njia ya haya kubwa kuvimba,au kutokeza uvimbe mkubwa kwa chini


- Mtu kushindwa kudhibiti haja kubwa na kujisaidia mwenyewe


- Kupatwa miwasho na hali kama ya kuchoma njia ya haja kubwa


MATIBABU YA UGONJWA HUU


- kansa hii huhusisha matibabu ya aina mbali mbali kama vile;matumizi ya dawa mbali mbali,huduma ya chemotherapy,Mionzi pamoja na Upasuaji.


KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!