KIFUNGUA KINYWA
• • • • •
KIFUNGUA KINYWA CHA ASUBUHI(CHAI) NI MUHIMU SANA MWILINI
Wataalam wa afya ya Binadamu pamoja na watu wa Lishe hushauri mtu kula vizuri sana asubuhi hata kuliko muda mwingine wowote.
Hapa tunatumia slogani hii " Kula asubuhi kama Mfalme, kula mchana kama malikia na kula usiku kama Mtumwa"
Tukiwa na maana kwamba, muda ambao unatakiwa kula vizuri kuliko wakati mwingine wowote ni asubuhi, halafu mchana kidgo unaweza kupunguza na usku ndyo unatakiwa kupunguza sana ukitakiwa kula kidgo na vitu vyepesi tu.
Tofauti na watu wengi walivyozoea, kwamba asubuhi anaweza anywe chai au hata asinywe kabsa, halafu mchana ndyo anakula sana na wakati wa usku ndyo usiseme,hii kiafya sio ratiba nzuri.
KWA NINI UNASHAURIWA KULA VIZURI SANA ASUBUHI?
- Mwili wako hutumia sana kwa kiwango kikubwa Protein pamoja na virutubisho vyingine kama Calcium wakati wa usku katika kurekebisha mwili,kuponyesha seli zilizojeruhiwa, ukuaji wake N.k
Matumizi haya hufanyika kwa kiasi kikubwa wakati wa usiku kuliko muda mwingine wowote, hivo humfanya mtu akimka,asubuhi kuhitaji kurudisha vitu hivi kwa kiwango kikubwa.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!