KIPIMO CHA MIMBA KUENDELEA KUSOMA HATA BAADA YA MIMBA KUTOKA

 MIMBA

• • • •

KIPIMO CHA MIMBA KUENDELEA KUSOMA HATA BAADA YA MIMBA KUTOKA


Wanawake wengi huchanganyikiwa na kushindwa cha kufanya baada ya kipimo cha mimba kuendelea kusoma na kuonyesha kwamba wana mimba wakati Mimba imeshatoka.


FAHAMU KWANZA MAMBO HAYA KUHUSU KIPIMO CHA MIMBA


Kipimo cha mimba kwa Njia ya mkojo maarufu kama Urinary pregnancy test au UPT, Usomaji wake hutegemea uwepo wa kichocheo kinachojulikana kwa jina la Human gonadotrophin hormone (HCG) kwenye mkojo.


Kichocheo hichi cha hcg huzalishwa na Placenta au kondo la nyuma kisha kuingia moja kwa moja kwenye mkojo, Hivo uwepo wa kichocheo hiki kwenye mkojo ndyo usomaji wa kipimo chetu cha UPT.


KIPIMO CHA MIMBA KUENDELEA KUSOMA HATA BAADA YA MIMBA KUTOKA


Ujauzito unaweza ukawa umetoka lakini bado kichocheo cha HCG kipo kwenye mkojo, hivo kwa hali hii hata kama mimba imetoka, ukipima ujauzito kwa kutumia kifaa cha UPT bado kitaendelea kusoma na kuonyesha una mimba mpaka hapo kichocheo cha hcg kitakapoacha kuzalishwa na kondo la nyuma(placenta) na kuwepo ndani ya mkojo.


Hivo basi kwa tafsiri nyingine tunaweza kusema, mabadiliko ya vichocheo vyako vya mwili hutokea pale unaposhika mimba, na sio swala la siku moja vichocheo vyako vya mwili kurudi kwenye hali ya kawaida kama mwanzoni.


Utakuwa ni shahidi wa hili kwamba, mimba inaweza kuwa imetoka na ukipima haipo au kipimo kinaonyesha kwamba wewe sio mjamzito  lakini bado una dalili zote za mimba kama vile;


- Kupata kichefu chefu na kutapika


- Kutema mate sana


- kukojoa mara kwa mara


- Maziwa au matiti kujaa


- Kutokuona period yako

N.K


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


* Jinsi ya kutumia kipimo cha mimba ukiwa nyumbani (Somo linakuja)




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!