KISUKARI CHA MIMBA(chanzo,dalili na tiba)

 MIMBA

• • • •

KISUKARI CHA MIMBA(chanzo,dalili na tiba)


Kisukari cha mimba ambacho kwa kitaalam hujulikana kama Gestational Diabetes ni kisukari ambacho hutokea kipindi mama akiwa mjamzito tu, kabla ya hapo hakuwa na sukari na baada ya kujifungua huisha pia.  


Tatizo hili huhusisha kuwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kuliko kawaida kipindi cha ujauzito.


CHANZO CHA TATIZO LA KISUKARI CHA MIMBA


- Hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo huhusishwa na kusababisha tatizo hili la kisukari cha mimba, ila kuna baadhi ya sababu huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata kisukari wakati wa mimba kama vile;


✓ Mama mjamzito kuwa na shida ya uzito mkubwa kupita kiasi


✓ Mama mjamzito kuwa na tatizo la   Polycystic ovary syndrome (PCOS)


✓ Mama mjamzito kutofanya mazoezi yoyote yale kipindi cha ujauzito


✓ Mama mjamzito kuwa na tatizo hili kwenye mimba za nyuma,pia anakuwa kwenye hatari ya kupata tena


✓ Kuwa katika familia ambayo kuna mtu ambaye amewahi kupata shida hii


✓ Mama kujifungua mtoto mkubwa au big baby kwenye mimba zilizopita


DALILI ZA KISUKARI CHA MIMBA


- Tatizo hili la kisukari wakati wa ujauzito, kwa asilimia kubwa halionyeshi dalili zozote za nje kwa mama mjamzito zaidi ya kupimwa na kuonekana kuwa ana shida hyo.


Zipo dalili chache kama mama Kupata kiu sana ya maji pamoja na kukojoa sana mara kwa mara


MATIBABU YA KISUKARI CHA MIMBA


Matibabu ya tatizo hili ni pamoja na mama kupunguza kula vyakula ambavyo vina sukari nyingi, na kupewa dawa mbali mbali za kudhibiti kiwango cha sukari mwilini mpaka ajifungue.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!