MAGONJWA
• • • • •
KUAMBUKIZWA MAGONJWA WAKATI WA KUMHUDUMIA MGONJWA
Ni muhimu kufahamu kwamba mtu yeyote huweza kupata magonjwa wakati wa kumhudumia mgonjwa kama asipochukua tahadhari husika, iwe ni mtaalam wa afya hospitalini au ni mtu mwingine nyumbani akimhudumia mgonjwa.
Fahamu kwamba kuna baadhi ya magonjwa ambayo huweza kuambukizwa kwa Njia zinazohusu kitu chochote kinachotoka kwenye mwili wa Mgonjwa kama vile; Damu, Mate,jasho,au maji maji mengine ya mwili.
Baadhi ya magonjwa ambayo huweza kuambukizwa kwa njia hizo ni pamoja na, Ugonjwa wa corona, ugonjwa wa ukimwi, ugonjwa wa Homa ya Ini N.K
Ugonjwa kama Homa ya ini, unaweza kuupata baada ya kugusana na maji maji,mate,damu au jasho kutoka kwa mgonjwa.
Ugonjwa kama ukimwi unaweza kuupata endapo una kidonda au michubuko na sehemu hiyo ikaingiwa na damu ya mgonjwa wa shida hii.
Hivo basi, swala la kuambukizwa magonjwa wakati unamhudumia mgonjwa lipo, wala sio unyanyapaa, ni muhimu sana kujua unamhudumia mgonjwa wa aina gani na uchukue tahadhari gani.
Hivo basi, kuchukua tahadhari za kujikinga wakati wa kumhudumia mgonjwa ni muhimu sana.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!