DAMU
• • • • •
KUCHANGIA DAMU HAKUNA MADHARA(soma hapa)
Watu wengi au jamii nyingi zimekuwa zikishikilia dhana potofu kwamba uchangiaji damu una madhara makubwa mwilini, na mtu akichangia damu itamlazimu kufanya hivyo kila mara.
DHANA POTOFU KUHUSU UCHANGIAJI DAMU
-Mtu akichangia damu itasababisha damu kuongezeka kila mara na kumlazimu kutoa damu kila wakati kwenye maisha yake yote.
Dhana hii ni potofu na imekuwa ikiwapa shida sana watu wanaohamasisha mpango wa uchangiaji Damu Salama.
FAHAMU HILI; Kulingana na maumbile ya Mwanaume yalivyo, Mwanaume ana uwezo wa kuchangia damu kila baada ya Miezi 3 Bila kupata shida yoyote, Na mwanamke ana uwezo wa kuchangia damu kila baada ya Miezi 4 bila shida yoyote.
Kama mtu ana shida ya damu kuongezeka akutane na wataalam wa maswala ya Damu kuangalia kwanini chembe chembe zake za damu zinajizalisha kupita kiasi na kupata Tiba sahihi,Lakini atambue hakuna uhusiano wa kuchangia damu na damu kuongezeka kwa wingi.
Vitu ambavyo huzingatiwa wakati wa uchangiaji damu ni pamoja na Kupima Uzito wa mwili, Presha N.K.
EPUKA IMANI POTOFU CHANGIA DAMU OKOA MAISHA.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!