UHUSIANO WA KUKOSA NGUVU ZA KIUME NA MWANAMKE KUSHINDWA KUBEBA MIMBA

 UZAZI

• • • •

UHUSIANO WA KUKOSA NGUVU ZA KIUME NA MWANAMKE KUSHINDWA KUBEBA MIMBA


Watu wengi huchanganya hivi vitu viwili, kwamba kukosa nguvu za kiume ndyo kukosa uwezo wa kumpa mwanamke mimba.


Ukweli ni kwamba japo vitu hivi vinauhusiano wa karibu sana ila ni vitu viwili tofauti kabsa.


Kukosa nguvu za kiume sio kushindwa kumpa mwanamke mimba, Unaweza ukawa na tatizo la nguvu za kiume lakini uwezo wako wa kumpa mwanamke mimba bado ukawa pale pale.


Tatizo la mwanaume kushindwa kumpa mwanamke mimba kwa asilimia kubwa linahusu mbegu za mwanaume  ikiwa ni pamoja na; Ubora wa mbegu, uwezo wa mbegu kukaa muda mrefu bila kufa, uwezo wa mbegu kusafiri kwa haraka zaidi, kiwango cha mbegu ambacho mwanaume anakitoa;


Hapa nazungumzia tatizo la mwanaume kuzalisha kiwango kidogo sana cha mbegu ambapo kwa kitaalam hujulikana kama low sperm count.


Tatizo la nguvu za kiume huhisha uwezo wa uume kusimama vizuri, uwezo wa kufanya tendo la ndoa vizuri,uwezo wa kurudia tendo la ndoa N.k


Hivo basi kwa maelezo hayo nafikiri sasa unaweza kutofautisha vitu hivi viwili(nguvu za kiume pamoja na uwezo wa mwanaume kumpa mwanamke mimba) japo vinaweza kwenda pamoja.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!