KUNDI LA WATU AMBALO LIPO KWENYE HATARI YA KUPATA MAGONJWA YA ZINAA

   MAGONJWA YA ZINAA

• • • • • •

KUNDI LA WATU AMBALO LIPO KWENYE HATARI YA KUPATA MAGONJWA YA ZINAA


Magonjwa ya zinaa ni magonjwa ambayo huweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kujamiiana au kufanya ngono. 


Magonjwa hayo ni pamoja na; Ugonjwa wa Kisonono, ugonjwa wa kaswende, Ugonjwa wa Chlamydia, Ugonjwa wa ukimwi N.k


KUNDI LA WATU AMBALO LIPO KWENYE HATARI YA KUPATA MAGONJWA YA ZINAA NI PAMOJA NA;


- Wanaofanya ngono zembe, yaani wanaofanya mapenzi bila kutumia kinga kama condom za kike au za kiume


- Wanaojishirikisha na kufanya mapenzi kinyume na maumbile


- Wale ambao wana wapenzi wengi au kwa kitaalam tunasema multiple sexual partners


- Wanywaji wa pombe au walevi


- Watumiaji wa madawa mengine ya kulevya ikiwa ni pamoja na sindano za kujidunga


- Wavutaji wa sigara


- Wajawazito kutokana na kushuka kwa kinga ya mwili kipindi cha ujauzito,hivo mwili kushindwa kupambana na magonjwa, na magonjwa kuingia na kushambulia mwili kwa urahisi zaidi.

N.K



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!