MAAMBUKIZI YA BACTERIA UKENI NA VISABABISHI VYAKE

 AFYA TIPS

• • • • •

MAAMBUKIZI YA BACTERIA UKENI NA VISABABISHI VYAKE


Bacteria vaginosis ni tatizo ambalo huhusisha ukuaji wa kiwango kikubwa pamoja na mashambulizi ya bacteria kwenye sehemu za siri za mwanamke(ukeni).


ZIPO DALILI MBALI MBALI AMBAZO MWANAMKE MWENYE TATIZO HILI ATAONYESHA KAMA VILE;


• Kutokwa na uchafu wenye rangi ya njano,maziwa, pink N.K


• Uchafu huo huambatana na harufu kali ukeni wengine kama shombo ya samaki


• Kupatwa na hali ya miwasho sana ukeni


• Maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu


• Maumivu makali ya kiuno


• Kuhisi hali ya kuchomwa na mkojo wakati wa kukojoa


• Mwili kupata uchovu sana


• Joto la mwili kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa

N.K


VISABABISHI NA VIHATARISHI VYA KUPATA TATIZO HILI KA BACTERIA VAGINOSIS NI PAMOJA NA;


- Mtu kufanya mapenzi na watu wengi


- Mtu kufanya ngono zembe(mapenzi bila kinga)


- Tabia ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile


- Kuwa na matatizo mengine ambayo hushusha kinga yako ya mwili


- Kupungua kwa kiwango kikubwa bacteria wazuri ukeni wanaojulikana kwa jina la Lactobacilli bacteria


- Matumizi ya baadhi ya vitu vyenye kemikali ukeni kama baadhi ya sabuni,mafuta N.k


- matumizi ya vifaa mbali mbali ukeni kama vile Sex toys N.K


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!