MADHARA YA KUBEBA MIMBA UKIWA UNANYONYESHA

 MIMBA

• • • •

MADHARA YA KUBEBA MIMBA UKIWA UNANYONYESHA


Watu wengi hawafahamu kwamba kuna madhara ya kubeba mimba ukiwa unanyonyesha. Licha ya hivyo, kuna watu wengi pia hawafahamu kwamba unaweza kubeba mimba nyingine hata kama ndyo bado una mtoto mdogo.


Uwezo wa mwanamke kubeba mimba hurejea baada tu ya mzunguko wake wa hedhi kurudi katika hali yake yakawaida hata kabla ya kuona siku zake. Kwani kinachotangulia ni yai kupevushwa na kutoka kwenye vifuko vyake yaani Ovaries kisha kuja kwenye mirija ya uzazi tayari kabsa kwa urutubishaji,ndipo baadae period ianze kutoka kama yai halikufanikiwa kurutubishwa.


MADHARA YA KUBEBA MIMBA UKIWA UNANYONYESHA


Unashauriwa kukaa angalau Miaka 2 au 3 Ndipo ubebe mimba nyingine na kuzaa tena. Yapo madhara mbali mbali ambayo huweza kutokea baada ya mwanamke kubeba mimba wakati bado ananyonyesha. Madhara hayo ni kama vile;


- Unakuwa kwenye hatari ya kuzaa mtoto kabla ya kukomaa yaani kwa kitaalam tunaita Premature baby


- Unakuwa kwenye hatari ya kuzaa mtoto mwenye shida ya uzito mdogo sana


- Wewe mwenyewe afya yako inakuwa dhoofu zaidi


- Unakuwa kwenye hatari ya kuzaa mtoto na kufariki


- Unakuwa kwenye hatari ya kuishiwa nguvu wakati wa kujifungua


- Unakuwa kwenye hatari ya kushindwa kuwapa watoto mahitaji yao kila wakihitaji ikiwa ni pamoja maziwa yao


- Wewe mwenyewe unaweza kuwa katika hatari ya kupoteza maisha


KUMBUKA; kupanga uzazi ni muhimu sana kwa ajili ya afya yako pamoja na afya ya watoto wako.


KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!