DAWA
• • • •
MADHARA YA KUOVERDOSE DAWA YA ibuprofen
Ibuprofen ni dawa ambayo watu wengi huitumia mara kwa mara pale wakiwa na tatizo la maumivu mbali mbali mwilini.
Dawa ya Ibuprofen mara nyingi hutumika kwa watu wenye matatizo ya;
- Maumivu makali ya kichwa
- Maumivu ya mgongo
- Maumivu makali wakati wa hedhi kwa wanawake
- Maumivu ya jino
- Maumivu ya mifupa
- Joto la mwili likiwa juu au mtu akiwa na Homa
N.k
Kumbuka; Mtoto ambaye ana umri wa chini ya miezi sita haruhusiwi kabsa kupewa dawa ya Ibuprofen
MADHARA YA KUOVERDOSE DAWA YA ibuprofen
- Matumizi ya zaidi ya kiwango cha mg 800 kwa mara moja au kiwango cha 3,200 mg kwa siku kwa mtu mzima, huweza kusababisha madhara makubwa mwilini kama vile;
• Mtu kuwa katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo
• Mtu kuwa katika hatari ya kupata matatizo ya Figo
• Mtu kuwa katika hatari ya kupata matatizo kwenye mfumo mzima wa chakula ikiwa ni pamoja na utumbo wote
• Mtu kuwa katika hatari ya kupata matatizo kwenye Ini
1. Hupata hali ya kichefuchefu pamoja na kutapika
2. Kupata hali ya kiungulia au heartburn
3. Kusikia sauti au kelele masikioni hali ambayo hujulikana kama tinnitus(ringing in the Ears)
4. Kupata kizunguzungu kikali
5. Kuharisha
N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!