MADHARA YA MWANAMKE KUVUTA SIGARA

SIGARA

• • • • • •

MADHARA YA MWANAMKE KUVUTA SIGARA


Madhara ya uvutaji wa sigara ni kwa kila mtu anayevuta bila kujalisha umri au jinsia, japo kuna madhara mengine huwa maalum kwa jinsia flani, Katika makala iliyopita nilielezea madhara ya Sigara kwa wanaume soma hapa..!!



Lakini katika makala ya leo tunazungumzia madhara ya Uvutaji wa sigara Kwa Wanawake.


MADHARA YA MWANAMKE KUVUTA SIGARA NI PAMOJA NA;


1. Uvutaji wa sigara huweza kumuweka mwanamke katika hatari ya kupata shida ya mimba kutunga nje ya kizazi yaani kwa kitaalam tunaita Ectopic pregnancy


2. Uvutaji wa sigara kwa mwanamke huweza kumsababishia kuwa katika hatari ya kupatwa na shida ya kansa mbali mbali


3. Mwanamke kuzaa watoto wenye tatizo la uzito mdogo sana kuliko kawaida(uzito wa kawaida Kgs 2.5 mpaka 3.5)


4. Mwanamke kuwa katika hatari ya kupatwa na tatizo la mvuruguko wa vichocheo vya mwili yaani kwa kitaalam tunaita hormone imbalance


5. Mwanamke kupatwa na shida ya kutokubeba mimba au kushika ujauzito na kutoka wenyewe


6. Kuzaa watoto wenye matatizo katika mfumo mzima wa upumuaji


7. Mwanamke kuzaa watoto wenye shida ya figo


8. Mwanamke kuzaa watoto na kufariki muda mfupi baada ya kuzaliwa


9. Uvutaji wa sigara huweza kusababisha matatizo ya mapafu ikiwa ni pamoja na Kansa ya mapafu


10. Kupatwa na shida ya koo ikiwa ni pamoja na kupatwa na kansa ya Koo

N.K


ONYO; uvutaji wa Sigara ni hatari kwa afya yako na afya ya mtoto wako


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!