SUMUKUVU
• • • • •
MADHARA YA SUMUKUVU MWILINI
Je Sumukuvu ni nini?
Sumukuvu ni aina ya Kemikali ambayo huzalishwa na Jamii ya Fangasi, Na fangasi hawa hupenda kuwepo kwenye mazao mbali mbali kama vile; Kwenye punje za Mahindi, karanga,kunde,mbegu za mafuta n.k
kemikali hii huweza kuleta athari kubwa kwa Binadamu pamoja na mifugo ambayo itakula mimea yenye Sumukuvu.
RIPOTI ya Wizara ya Afya Mwaka 2016, ilisema kwamba " Kati ya kipindi cha Juni mpaka Agosti 2016, Watu 68 waliathiriwa na Sumukuvu ambapo vifo 19 viliripotiwa katika mikoa ya DODOMA na MANYARA"
MADHARA YA SUMU KUVU MWILINI NI PAMOJA NA;
✓ Kusababisha vifo kwa binadamu pamoja na Mifugo
✓ Kuleta athari kubwa kwenye Ini
✓ Kusababisha maumivu makali ya Tumbo
✓ Kusababisha hali ya kutapika
✓ Kusababisha mtu kuharisha damu
✓ Kusababisha tatizo la kuvimba tumbo
✓ Kusababisha tatizo la kuvimba Miguu
✓ Kusababisha joto la mwili kuwa juu au Mtu kuwa na Homa
✓ Kusababisha rangi ya ngozi,macho,viganja vya mikono kuwa na rangi ya Manjano
✓ Kusababisha tatizo la Degedege
n.k
KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!