MATUMIZI YA CATHETER PAMOJA NA UTUNZAJI WAKE

 CATHETER

• • • • •

MATUMIZI YA CATHETER PAMOJA NA UTUNZAJI WAKE


Catheter ni kifaa ambacho hutumika kutoa Mkojo kwa Mgonjwa ambaye kwa namna moja au nyingine ni ngumu kukojoa mwenyewe au ni ngumu kutembea kwenda chooni kukojoa.


Catheter ina sehemu ya kuchomeka kwa mgonjwa pamoja na sehemu ya kuhifadhi mkojo maarufu kama catheter urinary bag.


Hivo basi matumizi ya catheter humsaidia sana mgonjwa ambaye hajiwezi, lakini pia zipo aina mbali mbali za catheter kama vile; Male catheter au Condom catheter N.K


UTUNZAJI WA CATHETER


Endapo mgonjwa anatumia catheter haijalishi yupo mazingira ya hospitalini au nyumbani, lakini catheter isipotunzwa vizuri huweza kuwa chanzo kikubwa cha kusababisha magonjwa mengine kwa mtumiaji.


Vimelea vya magonjwa huweza kupenya moja kwa moja kwa kutumia catheter na kuingia kwenye mwili wa mgonjwa kwa kutumia njia ya mkojo,hivo usafi na utunzaji wa catheter ni muhimu sana.


Epuka kuweka chini catheter ya Mgonjwa, endapo mgonjwa anaweza kutembea mwenyewe basi anaweza kuishikilia catheter yake isiguse chini na endapo mgonjwa kalala kitandani basi catheter ifungwe kitandani hasa urinary bag hufungwa vizuri kitandani.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!