MATUMIZI YA DAWA ZA PRESHA(ushauri)

 AFYA BORA

• • • • • • 

MATUMIZI YA DAWA ZA PRESHA(ushauri)


Kwa Mgonjwa wa Presha iwe ni presha ya kupanda au presha ya kushuka,nidhahiri kwamba muda mwingi huweza kutumia dawa ili kudhibiti kiwango cha Presha mwilini.


TABIA HATARISHI KWA MGONJWA WA PRESHA


Ni pamoja na matumizi ya dawa bila kupima na kujua presha yako ipo kwa kiwango gani mwilini.


Ingiwaje kwa wagonjwa wa presha kwa mda mrefu hufahamu dalili mbali mbali endapo presha ikiwa juu,ikiwa kawaida au ikishuka huweza kuhisi na kujua kama ipoje.


USHAURI KWA MGONJWA WA PRESHA


Iwe ni presha ya kupanda au presha ya kushuka ni vizuri kufanya vipimo kwanza au kupima kwanza na kujua presha yako ipo kwa kiwango gani ndipo ufanye uamuzi wa kutumia au kutokutumia  dawa flani za presha.


Wagonjwa wengi wa presha hununua vifaa maalum vya kupimia presha, hivo kuwa rahisi kufwatilia na kudhibiti kiwango cha presha mwilini hata wakiwa nyumbani.


Njia hii ni nzuri sana kwani itarahisisha ufwatiliaji wa presha kwenye mwili wako hata kabla ya kwenda hospital.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!