KISUKARI
• • • • •
MATUMIZI YA DAWA ZA UGONJWA WA SUKARI(ushauri)
Kama inavyofahamika ugonjwa wa sukari huhusisha kuwepo kwa kiwango kikubwa au kidogo sana kuliko kiwango cha wastani cha sukari ndani ya damu.
Ambapo wastani wa kiwango cha kawaida cha sukari ndani ya damu kwa watu wengi huwa kati ya 4.0 mmol/L mpaka 5.4 mmol/L wakiwa na njaa, Na mpaka 7.8 mmol/L masaa mawili baada ya kula chakula.
Hivo basi, kutokana na wastani wa viwango hivi vya sukari kwenye Damu, kuna sukari ya kupanda na sukari ya kushuka.
MATUMIZI YA DAWA ZA UGONJWA WA SUKARI
- Angalizo pamoja na Ushauri kuhusu matumizi ya dawa za ugonjwa wa sukari;
Matumizi ya dawa za ugonjwa wa sukari yaende sambamba na upimaji wa kiwango cha sukari kwenye damu
Hivo basi unashauriwa kupima kwanza kiwango cha sukari kwenye damu kabla ya kutumia dawa yoyote ya sukari
FAIDA YAKE; Ukipima sukari kabla ya kutumia dawa yoyote utajua kiwango cha sukari kwenye damu kabla ya dawa, na kukusaidia kuepuka madhara ya kushusha zaidi kiwango cha sukari kwenye damu kwa kutumia dawa za kushusha sukari wakati tayari imeshuka au
Kupandisha kiwango cha sukari kwenye damu zaidi wakati tayari kipo juu baada ya kutumia dawa za kupandisha kiwango cha sukari bila wewe kujua hali halisi kwenye mwili wako.
KUMBUKA; Kinga ni bora kuliko tiba, hivo usitumie dawa yoyote ya ugonjwa wa Sukari kabla ya kupima kiwango cha sukari kwenye damu.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!