MTOTO KUOTA VIPELE KWENYE NGOZI NA KUJIKUNA

 AFYA KWA MTOTO

• • • • • •

MTOTO KUOTA VIPELE KWENYE NGOZI NA KUJIKUNA


Tatizo hili la mtoto kuota vipele vingi kwenye ngozi pamoja na kujikuna sana hutokea kwa watoto wengi, huku wengine hadi kufikia hatua ya Ngozi ya mwili kubadilika rangi na kuwa na mabaka mabaka mekundu kila mahali.


Je tatizo hili hutokana na nini? na je nini kifanyike kwa watoto wenye matatizo kama haya? soma hapa..!!


CHANZO CHA TATIZO HILI


- Kuna sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia tatizo hili la mtoto kupata vipele kwenye ngozi pamoja na kujikuna sana, na baadhi ya sababu hizo ni kama vile;


• Kuna vipele ambavyo hutokana na hali ya joto kali


• Kuna vipele ambavyo hutokana na Allergy ya vitu mbali mbali kama vile mafuta ya Kupaka n.k


• Kuna vipele ambavyo hutokana na reaction ya mfumo wa kinga ya mwili kwa mtoto mwenyewe


• Kuna vipele pamoja na miwasho kwenye ngozi kutokana na maambukizi ya Fangasi wa Ngozi


• Pia magonjwa mbali mbali ya ngozi huweza kusababisha tatizo hili


ANGALIZO; Mama au mlezi unaweza kumchunguza mtoto wako na kuwa muangalifu kwa sababu, kuna hali ya mikwaruzo,ngozi ya mtoto kubadilika rangi na kuwa nyekundu kutokana na mtoto mwenyewe kujiparua kila mara.


MATIBABU YA TATIZO HILI


- Tiba sahihi ya tatizo hili huanza na kujua chanzo chake. Hivo mpeleke mtoto hospital ili akutane na wataalam wa afya kwa Watoto,wamchunguze mtoto kisha kuanza matibabu kama ni tatizo ambalo huhitaji matibabu.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!