MONGOLIAN SPOT
• • • • •
MTOTO KUZALIWA NA MABAKA MABAKA MAKALIONI NA MGONGONI(mongolian spot)
Mtoto huweza kuzaliwa akiwa na mabaka mabaka ya rangi ya blue hasa hasa maeneo ya makalioni na mgongoni, mabaka mabaka haya kwa kitaalam hujulikana kama Mongolian spot.
MABAKA MABAKA HAYA HUDUMU KWA MUDA GANI?
Mabaka mabaka(mongolian spot) huweza kupotea yenyewe ndani ya muda mfupi au kudumu kwa kipindi kirefu hata miaka Minne na kuendelea,
Kwa wengine hupotea yenyewe baada ya mtoto kufikia umri wa kubalehe Na baadhi ya watoto wachache mabaka mabaka haya huendelea kuwepo maisha yao yote.
CHANZO CHA MABAKA MABAKA HAYA NI NINI?
- Chanzo cha mabaka mabaka haya au Mongolian spot, ni kutokana na uwepo mkubwa wa seli hai kwa ajili ya kuleta rangi kwenye ngozi maarufu kama melanocytes hasa hasa maeneo ya makalioni na mgongoni,
ndyo sababu kubwa ya rangi ya ngozi katika maeneo haya kubadilika na kuwa blue kutokana na uwepo wa kiwango kikubwa cha Melanocytes ambazo huzalisha melanin(kwa ajli ya kuipa ngozi rangi yake).
MATIBABU YA MONGOLIAN SPOT
- Tatizo hili kwa mtoto huweza kuisha lenyewe wala hakuna matibabu yoyote ambayo hufanyika kwa mtoto mwenye shida hii kwenye ngozi yake
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE LA KIAFYA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!