MTOTO KUZALIWA NA UDHAIFU WOWOTE(chanzo)

 MTOTO

• • • •

MTOTO KUZALIWA NA UDHAIFU WOWOTE(chanzo)


Hali ya mtoto kuzaliwa na udhaifu wowote mfano; mtoto kuzaliwa na kichwa kikubwa,mtoto kuzaliwa na shida ya mgongo wazi, mtoto kuzaliwa na kichwa kidogo sana, mtoto kuzaliwa na mdomo wa sungura, Mtoto kuzaliwa na ulemavu wa miguu N.k 


Vyote hivi chanzo chake ni wakati wa uumbaji wa mtoto ambao unatokea katika miezi mitatu ya mwanzoni ya ujauzito ambapo kwa kitaalam tunasema " organogenesis occurs in first trimester of pregnancy"


Hivo shida yoyote kwa mtoto huanzia wakati wa uumbaji wake, na tafiti zinaonyesha zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia watoto kuzaliwa na matatizo.


CHANZO CHA WATOTO KUZALIWA NA MATATIZO MBALI MBALI NI PAMOJA NA;


1. Matumizi ya pombe wakati wa ujauzito


2. Mama mjamzito kuvuta sigara


3. Matumizi ya dawa ambazo haziruhusiwi kipindi cha ujauzito hasa hasa ile miezi mitatu ya mwanzoni ambapo ndyo uumbaji wa mtoto hufanyika


4. Kuwa na matatizo ya ugonjwa wa kisukari kabla na wakati wa ujauzito ambacho hakijadhibitiwa vizuri


5. Kuwa na tatizo la uzito kupita kiasi au Obesity


6. Kubeba ujauzito katika umri mkubwa sana


7. Kuwa na vinasaba vya tatizo flani ndani ya ukoo wenu au famili yenu hivo kumrithisha na mtoto pia.


EPUKA HAYA WAKATI WA UJAUZITO;


- Matumizi ya dawa hovio bila maelekezo kutoka kwa wataalam wa afya


- Matumizi ya pombe wakati wa ujauzito


- Uvutaji wa sigara wakati wa ujauzito

N.k


Matumizi ya vidonge vyekundu vya kuongeza damu maarufu kama FEFOL au Folic acid husaidia katika uumbaji wa mtoto ikiwa ni pamoja na kupunguza idadi ya watoto kuzaliwa na shida ya vichwa vikubwa pamoja na Mgongo wazi, mbali na kuongeza damu ya mama.


KUMBUKA; uzazi salama unawezekana na unaanzia kwako,chukua hatua sasa



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!