UKIMWI
• • • • •
NINI CHA KUFANYA BAADA YA KUFANYA MAPENZI NA MUATHIRIKA WA UKIMWI?
Wapo baadhi ya watu,wanaume kwa wanawake huingiwa na wasi wasi mkubwa baada ya kugundua kwamba watu ambao wameshiriki nao tendo la Ndoa ni Waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi.
Hofu hii huja baada ya kushiriki tendo la ndoa,ndipo baadae Mmoja wa washiriki hawa agundue mwenzake ameathirika.
NINI CHA KUFANYA BAADA YA KUFANYA MAPENZI NA MUATHIRIKA WA UKIMWI?
Fanya mambo haya yafuatayo baada ya kugundua kwamba, uliye fanya naye mapenzi ni muathirika wa ukimwi;
- Nenda hospital kafanye vipimo vya awali kwanza
- Hakikisha unarudia kupima tena baada ya Miezi mitatu
Kumbuka; Hata kama umepata maambukizi ya Virusi vya ukimwi leo, vipimo haviwezi kuonyesha kwa muda huu huu
Asilimia 98% ya maambukizi ya virusi vya ukimwi huonekana kwenye kipimo baada ya miezi mitatu.
Hivo ni lazima kuridia tena vipimo,ili kujua kama upo salama au umeambukizwa.
KUMBUKA; Sio kila aliyefanya mapenzi na muathirika wa ukimwi tayari ana ukimwi
- Zingatia kinga wakati wa kufanya mapenzi(Condom)
- epuka kuwa na wapenzi wengi
KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!