SABABU ZA MENO KUBADILIKA RANGI

 MENO

• • • • •

SABABU ZA MENO KUBADILIKA RANGI


Bila shaka wewe ni mmojawapo ambaye una shida hii ya meno kubadilika rangi au umekutana na mtu mwenye Meno ambayo rangi ipo kwenye picha hapo chini.


Watu wengi kutoka maeneo ya Singida,Moshi na Arusha huwa wana meno ambayo rangi yake imebadilika na kuwa kama kwenye picha hapo chini. Je nini chanzo chake?


SABABU ZA MENO KUBADILIKA RANGI NI PAMOJA NA;


✓ Matumizi ya maji ambayo yana kiwango kikubwa cha madini ya Fluoride Kuanzia utoto wako nakusababisha hali ambayo hujulikana kama dental Fluorosis


✓ kula chakula au vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha Carbon


✓ Mama mjamzito kutumia dawa aina ya Tetracycline wakati uumbaji wa mtoto ndyo unafanyika hasa meno ya mtoto yakiwa yanaumbwa huku kukiwa na ukosefu mkubwa wa madini


✓ Uvutaji wa sigara kwa muda mrefu huweza kusababisha meno ya juu kubadilika rangi


✓ Kuumia,kugonjwa au kupata ajili yoyote ambayo huhusisha meno, huweza kupelekea sehemu hai ya meno kufa na kusababisha meno kubadilika rangi


✓ Udhaifu ambao huweza kutokea wakati wa uumbaji wa meno hali ambayo huweza kupelekea meno ya juu kunadilika rangi. Udhaifu huu kwa kitaalam hujulikana kama amelogenesis imperfecta 


✓ Matibabu yoyote ya meno ambayo yalihusisha mizizi yake huweza kupekea meno kubadilika rangi


MATIBABU YA TATIZO LA MENO KUBADILIKA RANGI


- Matibabu ya tatizo hili huhusisha njia mbali mbali kama vile kubadilisha rangi za meno kwa kung'arisha nje au ndani ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Internal or External Bleaching.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!