SABABU ZA MTOTO KUACHA KUCHEZA TUMBONI(mjamzito)

UZAZI

• • • • • •

SABABU ZA MTOTO  KUACHA KUCHEZA TUMBONI(mjamzito)


Mama ambaye ujauzito wake umefikia umri wa mtoto kucheza tumboni anatakiwa kumsikia mtoto akicheza kila siku, Hali ya mtoto kuacha kucheza kwa zaidi ya masaa 24 ni dalili ya hatari hivo unatakiwa kwenda hospital mara moja.


Wanawake wengi wajawazito mtoto huanza kucheza kuanzia wiki ya 24 huku wengine wakiwahi zaidi au wengine wakichelewa kulingana na sababu moja au nyingine, ikiwa ni pamoja na idadi ya watoto au mimba ambazo umewahi kupata N.K.


Je kama mtoto kutokucheza tumboni kwa zaidi ya masaa 24 ni dalili ya hatari,kipi kinasababisha hali hii kwa mjamzito?


SABABU ZA MTOTO  KUACHA KUCHEZA TUMBONI(mjamzito)


1. Mtoto kufia tumboni bila mama kujua

2. Mtoto kukosa nguvu kutokana na kukosa chakula chakutosha tumboni

3. Mama kuwa na matatizo mbali mbali wakati wa ujauzito kama vile tatizo la mama kuishiwa na pumzi kabsa hadi kufikia hatua ya kuwekewa mipira ya oxygen

4. Mtoto kukosa hewa ya kutosha tumboni kutokana na mama mwenyewe kushindwa kupitisha hewa ya kutosha kwenda kwa mtoto

5. Mama kuwa na shida kwenye mfumo wake wa damu ikiwa ni pamoja na kuwa na kansa ya damu N.K

6. Kondo la nyuma yaani placenta kuachia sehemu ambapo limejishikiza, hivo kukata mawasiliano kati ya mama na mtoto hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Placenta abruption


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!