SABABU ZA MWANAMKE KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI

 UZAZI

• • • •

SABABU ZA MWANAMKE KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI



 ZIPO SABABU MBALI MBALI AMBAZO HUCHANGIA MWANAMKE KUJIFUNGUA KWA NJIA YA UPASUAJI(OPERATION)


➡️ Ombeni Mkumbwa


Kumekuwa na Ongezeko kubwa la Wanawake wengi Kujifungua Kwa Njia ya Upasuaji au Operation katika siku za Hivi Karibu,Huku tatizo hili Likichangiwa na Sababu Mbali mbali kama Vile;


1. Mtoto kuwa Mkubwa kuliko Njia ya Kujifungulia au Njia kuwa Ndogo kuliko size ya Mtoto,ambapo kwa kitaalam Hujulikana kama CEPHALOPELVIC DISPROPORTION(CPD)


2. Mama Kuishiwa Nguvu na Kushindwa Kusukuma Mtoto hivo kupelekea kufanyiwa Upasuaji


3. Kondo la Nyuma kuachia kutoka sehemu lilipojishikiza ambapo kitaalam hujulikana kama Placenta abruption


4. Kondo la Nyuma Kushuka na Kufunika Njia Ya Mtoto kupita ambapo kitaalam hujulikana kama Placenta previa


5. Mama Kupatwa na Kifafa Cha Mimba wakati wa Ujauzito


6. Mapigo ya mtoto kupungua au kushindwa kupumua na matatizo mengine ndani ya tumbo la Uzazi ambapo kitaalam Hujulikana kama Fetal Distress


7. Mama mwenyewe Kuomba Kufanyiwa Upasuaji kwa Sababu zake Binafsi


8. Njia kushindwa Kufunguka Ili mtoto azaliwe


KUMBUKA; Ni muhimu sana kwa Mama Mjamzito kwenda Kliniki ili kupata vipimo vyote sahihi, na hata kugungulika kwa Dalili za Hatari Kwa Mjamzito mapema,na kupata matibabu sahihi ili kuepusha madhara ambayo huweza Kujitokeza.


@Kwa Ushauri zaidi,Elimu, Au Tiba tuwasiliane kwa Namba +255758286584


Karibu Sana..!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!