SABABU ZA PID KURUDI MARA KWA MARA BAADA YA MATIBABU

 PID

• • • • •

SABABU ZA PID KURUDI MARA KWA MARA BAADA YA MATIBABU


Pid ni kifupi cha maneno haya "Pelvic Inflammatory disease" ikiwa na maana ya maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke.


SABABU ZA PID KURUDI MARA KWA MARA BAADA YA MATIBABU


1. Sababu kubwa ni mwanamke kuanza kushiriki mapenzi au tendo la ndoa wakati bado yupo kwenye dose ya dawa au mara tu baada ya kumaliza dawa na kuanza kufanya mapenzi.


Tabia hii huweza kusababisha PID kurudi upya hata kama ulikuwa kwenye matibabu.


2. Inashauriwa kwamba, hata kama PID imegundulika kwa mwanamke, basi na mwanaume ambaye yupo kwenye mahusiano na mwanamke huyo lazima na yeye aanze matibabu.


Bila hivo mwanaume atakuwa anahifadhi vimelea vya Ugonjwa wa PID na hata mwanamke akipona baada tu ya kufanya mapenzi na mwanaume huyu, hurudisha tena vimelea vya ugonjwa huu wa PID.


Hivo kupelekea ugonjwa wa PID kurudi tena hata kama ndyo umemaliza matibabu.


BAADHI YA DALILI ZA PID NI PAMOJA NA;


- Maumivu wakati wa kufanya mapenzi


- Mwanamke kukauka sana sehemu za siri


- Mwanamke kuvuja maji maji mara kwa mara ukeni yenye harufu mbaya


- Mwanamke kutoa uchafu wenye rangi ya Njano


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!