TAMBUA NA FAHAMU MADHARA YA MATUMIZI YASIOFAA YA VIUAVIJASUMU (ANTIBIOTICS).
ANTIBIOTICS
• • • • • •
TAMBUA NA FAHAMU MADHARA YA MATUMIZI YASIOFAA YA VIUAVIJASUMU (ANTIBIOTICS).
DHANA HALISI
Viuavijasumu (antibiotics) ni dawa zinazotumika kutibu magonjwa mbali mbali yasababishwayo na bacteria, Protozoa, Micro plasma, Fungal n.k hivyo dawa hizo hutibu magonjwa kwa kuua bacteria na kuzuia kuzaliana Kwa bacteria mwilini.Pia inazuia kuzaliana tu kwa baadhi (Sio wote) ya virusi na sio kuwaua kabisa.
Mfano wa dawa hizi ni ampicillin, ciprofloxacin, tetracycline, gentamycin, Pen V, erythromycin, metronidazole, Amoxillin.
CHANGAMOTO YA USUGU WA DAWA.
Moja ya changamoto kubwa katika matibabu ni pale baadhi ya bacteria wanapojenga usugu dhidi ya dawa hizi. Kijiuasumu kikitumiwa kwa mda mrefu baadhi ya bacteria hujenga usugu ya dawa hizo na hivyo kutokuwawa na kijiuasumu hicho.
Ugonjwa unaotokana na bacteria hawa unakuwa mgumu kutibika na unaweza kuambukizwa kwa watu wengine. Ili kutibu ugonjwa unaotokana na bacteria hawa sugu unahitaji dawa yenye nguvu zaidi na uangalizi wa hali ya juu.
MADHARA YA KUTUMIA ANTIBIOTICS KIHOLELA.
Ingawaje vijiuasumu ni muhimu katika matibabu ya magonjwa mbali mbali kama zikitumiwa ipasavyo, lakini matumizi mabaya huleta madhara kwa mtumiaji;-
1) Inafanya mwilini kuwa sugu na dawa za antibiotic (Resist).
2) Inawafanya baadhi ya vimeelea wa magonjwa kuwa sugu (Resistance) na kutoangamizwa na dawa zinapotumika kama tiba.
3) Inavuruga mpangilio (chain) ya ufanyaji kazi wa kinga za mwili (Body Immunity) na hivyo kupunguza kinga za mwili.
MATUMIZI YASIYOSAHIHI YA ANTIBIOTICS
Mifano ya matumizi yasiyosahihi ya vijiua sumu:
1) Kutotumia dozi kamili ya vijiuasumu na kwa muda uliolekezwa.
2) Kutumia vijiuasumu kutibu magonjwa yasiyohitaji vijiuasumu kwa mfano ugonjwa kama mafua ambao husababishwa na virusi au aleji.
3) Kutumia dawa zinazokinzana kiutendaji kwa pamoja, kwa mfano baadhi ya vijiuasumu na vidonge vya uzazi wa mpango.
4) Kunywa pombe wakati ukiwa kwenye dozi ya dawa ambapo ulishauliwa usinywe pombe.
5) Kununua kiholela na kutumia dawa bila kufanyiwa uchunguzi.
6) Kutumia dozi isiyo sahihi.
NUKUU:
Ili kuepuka au kupunguza kutokea na usugu wa bacteria unashauriwa kutumia dawa zako kwa usahihi. Cr: Dr.Sam
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!