TATIZO LA ALDOSTERONISM(chanzo,dalili,tiba)

 TATIZO LA VICHOCHEO MWILINI

• • • • •

TATIZO LA ALDOSTERONISM(chanzo,dalili,tiba)


Aldosteronism hili ni tatizo ambalo huhusisha tezi aina ya Adrenal Gland kuzalisha  kwa kiasi kikubwa sana kichocheo aina ya Aldosterone kuliko ilivyokawaida.


CHANZO CHA TATIZO LA ALDOSTERONISM


- Kurithi vinasaba vya tatizo hili ndani ya familia au koo flani


- Kufanya kazi kupita kiasi kwa tezi zote mbili za Adrenal Gland


- Kuwa na shida ya kansa kwenye tezi moja au mbili ya adrenal Gland


- N.K



DALILI ZA TATIZO LA ALDOSTERONISM NI PAMOJA NA;


- Mgonjwa kupata kiu sana ya maji


- Mgonjwa kupata hisia za kukojoa kila mara


- Mwili kuchoka kupita kiasi


- Kuwa na shida ya presha kuwa juu


- Kuwa na tatizo la Kukaza kwa misuli ya mwili


- Kupata maumivu makali ya kichwa mara kwa mara

N.K


MATIBABU YA TATIZO LA ALDOSTERONISM


✓ matibabu ya tatizo hili hutegemea na chanzo chake,ila kwa ujumla zipo tiba mbali mbali kama vile;


 matumizi ya dawa zinazozuia uzalishwaji wa kiwango kikibwa cha hormone ya Aldosterone pamoja na Kufanyiwa upasuaji na kuondolewa kwa tezi hizi.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!