GEOGRAPHICAL TONGUE
• • • • •
TATIZO LA GEOGRAPHICAL TONGUE(chanzo,dalili na Tiba)
Geographical Tongue ni hali ya ulimi wa mtu kuchora kama ramani(mfano kwenye picha hapo chini), hali ambayo hutokea kwa baadhi ya Watu.
Hali hii haisababishi maumivu yoyote wala haina uhusiano na maambukizi ya Magonjwa ya Ulimi kama vile Fangasi wa ulimi N.K
CHANZO CHA TATIZO LA GEOGRAPHICAL TONGUE
- Hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo inajulikana kusababisha shida hii ya geographical tongue
DALILI ZA TATIZO LA GEOGRAPHICAL TONGUE
- Ulimi kuchora vitu kama ramani(tazama picha hapo chini)
- Hakuna maumivu yoyote kwenye ulimi
- Ila kwa baadhi ya watu huweza kuhisi hali ya ulimi kuchoma choma kwa sehemu ya mbele
MATIBABU YA SHIDA YA GEOGRAPHICAL TONGUE
- Hakuna tiba ya moja kwa moja kwa ajili ya kutibu hali hii, japo kwa mtu mwenye shida hii, kama unawasiwasi sana unaweza kuchunguzwa ili kuweza kuhakikisha kwamba ni geographical tongue na sio tatizo lingine
Shida hii haina madhara yoyote, na baadhi ya tafiti huonyesha kwamba hali hii huweza kuongesha uwezo wa ulimi kuhisi ladha za vitu mbali mbali
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!