INI
• • • • •
TATIZO LA INI KUFELI GAFLA(Acute liver failure)
Ini ni kiungo muhimu sana kwenye mwili wa binadamu ambacho hufanya kazi nyingi sana kuliko kiungo chochote, inakadiriwa kuwa ini huweza kufanya kazi zaidi ya 500 mwilini.
Acute liver failure ni tatizo ambalo huhusisha ini kupoteza uwezo wake wa kufanya kazi kwa gafla.
CHANZO CHA TATIZO HILI LA INI KUFELI GALFA(ACUTE LIVER FAILURE)
- Kuwa na matatizo kwenye mishipa ya damu ndani ya Ini
- Matumizi ya baadhi ya dawa kupita kiasi(Overdose) mfano wa dawa kama vile; Acetaminophen
- Kupatwa na ugonjwa wa kiharusi
- Mgonjwa kunywa sumu
- Magonjwa ya mfumo mzima wa mmeng'enyo wa chakula
- Kuwa na tatizo la kansa ya Ini
- Kuwa na shida ya Kinga ya mwili kupambana yenyewe yaani Autoimmune disease
N.K
DALILI ZA TATIZO LA INI KUFELI GAFLA(Acute liver failure)
✓ Kubadilika rangi ya ngozi na kuwa manjano pamoja na macho
✓ Kuvimba tumbo lako
✓ Kupata maumivu makali juu kidogo ya kitovu chako
✓ Mgonjwa kupatwa na hali ya mwili kutetemeka
✓ Mgonjwa kuhisi kichefuchefu pamoja na kutapika
✓ Mgonjwa kupata usingizi au kulala lala kila mara
✓ Kupata uchovu wa mwili kupita kiasi
N.K
MATIBABU YA TATIZO LA INI KUFELI GAFLA
- Tiba ya tatizo hili hutegemea na chanzo chake, ila kwa ujumla wake kuna matumizi ya dawa mbali mbali na endapo tatizo litakuwa kubwa sana basi mgonjwa huweza kufanyiwa Liver Transplant
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!