TATIZO LA KUJISAIDIA HAJA KUBWA BILA KUJIZUIA(fecal incontinence)

 FECAL INCONTINENCE

• • • • • • •

TATIZO LA KUJISAIDIA HAJA KUBWA BILA KUJIZUIA(fecal incontinence)


Tatizo la kujisaidia haja kubwa(kinyesi) pasipo ridhaa yako huweza kutokea kwa mtu yoyote na shida hii kwa kitaalam hujulikana kama Fecal Incontinence.


Zibo baadhi ya sababu ambazo huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupatwa na shida hii ya Fecal Incontinence(kujisaidia haja kubwa bila kujizuia)


Shida hii huweza kuwa ya muda mfupi na kuisha au huweza kuwa ni tatizo la muda mrefu pia.


CHANZO CHA TATIZO HILI


• Tatizo hili la mtu kujisaidia haja kubwa bila kupanga huweza kuchangiwa na sababu mbali mbali kama vile;


1. Kuharibika na kupoteza nguvu au uimara wa misuli maeneo ya njia ya haja kubwa katika kudhibiti haja kubwa kutoka


2. Kuharibika kwa mfumo mzima wa fahamu au Nerve system


3. Maambukizi ya magonjwa mbali mbali ikiwa ni pamoja na kansa ya eneo la haja kubwa


4. Kuwa na tatizo la Fistula ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Anal fistula


5. Kuwa na shida ya bawasiri kwa kitaalam hemorroids


6. Kuwa na uwezo mdogo wa kifuko cha kuhifadhia uchafu maarufu kama rectum kutokana na sababu mbali mbali kama vile upasuaji


7. Kuwa na tatizo la kuharisha


8. Mtu kuwa na tabia ya kujihusisha na mapenzi kinyume na maumbile yaani anal Sex mara kwa mara.

N.K


DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


✓ Mtu kujisiadia mwenyewe bila kupanga, na bila kujali yupo wapi au eneo gani


✓ Ambapo huambatana na matatizo mengine kama vile


- Kujisaidia kwa kuharisha


- Kupata maumivu makali ya tumbo


- Tumbo kujaa gesi na kunguruma


- Kupata shida wakati unataka kujisaidia kwa kupanga wewe


MATIBABU YA TATIZO HILI


Matibabu ya Tatizo hili la mtu kujisaidia mwenyewe bila kupanga yeye hutegemea na chanzo husika, hivo basi kwa ujumla wake matibabu ya shida hii huweza kuhusisha njia mbali mbali kama vile;


✓ aina ya mazoezi ya kukaza misuli ya njia ya haja kubwa


✓ Dawa mbali mbali za kutibu magonjwa

N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!