TATIZO LA KUSHINDWA KUMEZA KITU(dysphagia)

 KUMEZA

• • • • •

TATIZO LA KUSHINDWA KUMEZA KITU(dysphagia)


Tatizo la mtu kushindwa kumeza kitu chochote au kupata shida sana pamoja na maumivu makali wakati wa kumez kitu chochote, ni tatizo ambalo huweza kumpata mtu yoyote na kwa kitaalam tatizo hili hujulikana kama Dyphagia.


Shida inatokea pale kitu chochote kama vile chakula,maji,chai au kinywaji chochote kinapotaka kupita kutokea mdomoni kwenda tumboni.


CHANZO CHA TATIZO HILI


- Kushindwa kutanuka vizuri kwa njia ya chakula ili kuruhusu chakula kushuka unavyokula hali ambayo hujulikana kama Achalasia


- Kuwa na maambukizi ya magonjwa mbali mbali kama vile fangasi wa kooni


- Kuwa na tatizo la kansa ya kooni


- Kuwa na tatizo la uvimbe kwenye njia ya chakula


- Kuingia kwa kitu na kuziba njia ya chakula


- Kuwa na shida ya kuharibika kwa mfumo wa fahamu au nerves kwenye mwili wako

n.k


DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


1. Kupata shida ya kumeza kitu chochote


2. Kupata maumivu makali wakati wa kumeza kitu chochote


3. Kupata kiungua cha mara kwa mara (heartburn)


4. Kupata shida ya kupandisha chakula kila unavyokula


5. Kuhisi kama chakula au kitu ulichokula kuna sehemu kimekwama


6. Kukohoa kila unavyojaribu kumeza kitu chochote


7. Uzito wa mwili kushuka kwa kasi sana


MATIBABU YA TATIZO HILI


- Matibabu ya tatizo hili hutegemea na chanzo chake,ila kwa ujumla wake kuna baadhi ya njia huweza kutumika kutibu tatizo hili kama vile; 


Matumizi ya baadhi ya dawa za kutanua mfumo na njia ya chakula, Dawa za magonjwa mbali mbali kama vile fangasi wa kooni, Kufanya mazoezi maalumu ya kumsaidia mgonjwa aweze kumeza kitu bila shida, pamoja na huduma ya upasuaji.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!