Ticker

6/recent/ticker-posts

TATIZO LA KUTOA DAMU WAKATI WA KUFIKA MSHINDO KWA WANAUME(chanzo,dalili,tiba)



WANAUME

• • • • •

TATIZO LA KUTOA DAMU WAKATI WA KUFIKA MSHINDO KWA WANAUME(chanzo,dalili,tiba)


Sote tunajua kua kufika mshindo katika mapenzi ni jambo zuri na lenye furaha kubwa kwa mwanaume na mwanamke. Sasa wapo baadhi ya wanaume ambao wanapofika mshindo wanatoa damu au bao lenye damu. Matatizo haya sio ya kutisha wala kuogopa sana kwani asilimia 90 hutokea kwa sababu za kawaida na ambazo zinatibika vizuri kabisa. Asilimia chache ndo inaweza kua mambo makubwa kama saratani nk. Kwa mwanaume mwenye miaka chini ya 40 haatakiwi kabisa kua na wasiwasi kwani uwezekano wa kua na saratani ni mdogo sana.


Baadhi ya visababishi vya kutoa damu wakati wa mshindo ni👇🏾


1) Magonjwa ya zinaa kama kisonono na klamidia


2) kufanya mapenzi kila siku kwa zaidi ya wiki 2 (Frequent daily ejaculation over a period of several weeks)


3) Matatizo ya mishipa ya damu (Vascular malformations)


4) Kichocho (Schistosomiasis)


5) Saratani iliyosambaa kwenda kwenye via vya uzazi (metastatic Cancer)


6) Matatizo ya kuvuja damu(bleeding disorders) 


7) Uvimbe au saratani ya via vya uzazi 


VIPIMO KWA MWANAUME MWENYE DAMU KWENYE BAO

Mwanaume mweye damu kwenye bao akifika hospitali atasikilizwa kwa umakini,kuangaliwa na ndipo atafanyiwa vipimo ili kubaini chanzo. Kuna vipimo kama👇🏾


1) KUPIMA MKOJO(URINALYSIS)


2) KUPIMA SHAHAWA (SEMEN ANALYSIS)


3) KUPIMA PSA (ROUTINE PROSTATE-SPECIFIC ANTIGEN);Kwa wenye miaka 50 na kuendelea


4) KUPIMA ULTRASSOUND YA MFUMO WA UZAZI (TRANSRECTAL ULTRASOUND)-Hiki ndo kipimo cha kuangalia mfumo wa uzazi cha kwanza na cha uhakika. Ultrasound hii hufanyika kupitia njia ya haja kubwa


5) KUPIMA MRI YA MFUMO WA UZAZI (ENDORECTAL COIL MRI);Hiki ni kipimo kikubwa cha mfumo wa uzazi wa mwanaume. Kipimo hiki hufanyika kupitia njia ya haja kubwa


MATIBABU

Hali hii kwa asilimia kubwa huisha yenyewe hata bila ya matibabu. Kama matibabu yakihitajika basi ni kwa wale wagonjwa ambao hali hii imekua ikijirudia rudia au imekaa muda mrefu bila kuisha. Matibabu hutolewa kulingana na kinachosababisha hali hii.

Kwa kua hali hii sio ya hatari na huisha yenyewe kwa hio wanaume msiwe na wasiwasi na cha kujua ni kwamba itaisha na muwe na amani pale uonapo hali hii (Reassurance for most patients). Cr: @Drmathew








Post a Comment

0 Comments