TATIZO LA KUVIMBA MSHIPA MKUBWA WA AORTA TUMBONI(Abdominal aortic aneurysm)

MSHIPA

• • • • •

TATIZO LA KUVIMBA MSHIPA MKUBWA WA AORTA TUMBONI(Abdominal aortic aneurysm)


Abdominal aortic aneurysm ni tatizo ambalo huhusisha kuongezeka ukubwa wa mshipa mkubwa wa damu unaojulikana kwa jina la Aorta unaotokea kwenye moyo kushuka chini ya mwili.


CHANZO CHA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


- Kujaa kiasi kikubwa cha mafuta yaani Fatty na kuziba mshipa huu wa Aorta


- Kuwa na tatizo la shinikizo la damu au presha


- Kuwa na magonjwa mbali mbali ya Mishipa ya damu


- Kuumia kwenye eneo hili la mshipa


- Kupata maambukizi kwenye mishipa ya damu kwa kitaalam hujulikana kama blood vessel infections


- Kurithi vinasaba vya tatizo hili katika koo au familia flani

N.K


DALILI ZA UGONJWA HUU NI PAMOJA NA;


• Mgonjwa kupata maumivu makali sana ya tumbo


• Mgonjwa kupata maumivu makali sana ya mgongo


• Mgonjwa kuhisi mshipa kudunda maeneo ya kwenye kitovu


WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA TATIZO HILI


- Wenye umri mkubwa


- Wanaojihusisha sana na matumizi ya tumbaku


- Wanaume kuliko wanawake


- Watu ambao wapo kwenye familia yenye mgonjwa huyu


- Watu wenye ngozi nyeupe



VITU VYA KUEPUKA KUJIKINGA NA TATIZO HILI


✓ Epuka matumizi ya tumbaku


✓ Epuka kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha mafuta


✓ Fanya mazoezi angalau Dakika 30 kila siku


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!