TATIZO LA KUVUJA JASHO KUPITA KIASI(hyperhidrosis),chanzo,dalili na Tiba yake
AFYA YA MWILI
• • • • •
TATIZO LA KUVUJA JASHO KUPITA KIASI(hyperhidrosis)
Tatizo hili la mtu kuvuja jasho kupita kiasi ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Hyperhidrosis, hutokea pale ambapo hakuna vyanzo vyovyote ambavyo huweza kusababisha jasho, Mfano mtu kuchomwa na jua sana, Kufanya mazoezi n.k
Hali hii hutokea mtu akiwa katulia kabsa, kitu ambacho huwa ni kero kubwa kwake pamoja na kwa watu wengine ambao wapo karibu na yeye,
Mtu huyu huweza kuloa sana jasho mwili mzima ikiwa ni pamoja na maeneo mbali mbali kama vile; Usoni, Miguuni, Kwapani na Kwenye Mikono yake.
CHANZO CHA TATIZO HILI NI NINI?
• Chanzo cha kwanza cha tatizo hili, ni mfumo wa nerves mwilini kutuma taarifa kupita kiasi kwenda kwa tezi la Jasho yaani Sweat gland, hali ambayo hupelekea tezi hili kufanya kazi kupita kawaida,
Hasa hasa kukiwa hakuna mazingira yoyote ya joto,jua, au kitu chochote ambacho huweza kupasha mwili joto
• Mtu kuwa na maambukizi ya magonjwa mbali mbali,ambayo huweza kuupasha mwili joto kama vile Malaria n.k
• Kuwa na tatizo la Kisukari
• Kuwa na matatizo kwenye mfumo wa Fahamu au Nerves mwilini
• Mtu kupata shambulio la Moyo yaani Heart attack
• Kuwa na matatizo kwenye tezi la Thyroid
• Kuwa na tatizo la Saratani
• Hali hii pia huweza kutokea kwa wanawake ambayo wamefika ukomo wa hedhi yaani Menopause hot Flashes
DALILI ZA TATIZO HILI LA HYPERHIDROSIS
- Dalili kubwa ni mtu kutoa jasho kupita kawaida pasipo na chanzo chochote cha jasho kama vile jua,mazoezi n.k
- Mtu kutoa jasho kupita kiasi hadi kufikia hatua ya kukosa nguvu na kuishiwa maji ya mwilini
- Nguo kuloa sana wakati mtu akiwa kavaa, kama vile; Shati n.k
- Mtu kuvuja jasho sana wakati wa Usiku akiwa amelala
MATIBABU YA TATIZO HILI
✓ Matibabu ya tatizo hili hutegemea na chanzo chake, ila kwa ujumla kuna aina mbali mbali za dawa ambazo huweza kutumika kama vile; Antidepressants, antiperspirant dawa za magonjwa kama Malaria N.k
Epuka kukaa kwenye mazingira yoyote ambayo huweza kupasha mwili joto kama vile; Kukaa kwenye jua sana, kukaa karibu na Moto n.k
Hivo kutana na wataalam wa afya kwa ajili ya kupata msaada kama una tatizo hili.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!