TATIZO LA KUWASHWA MACHO(chanzo,dalili,madhara na tiba yake)

 MACHO

• • • • • 

TATIZO LA KUWASHWA MACHO(chanzo,dalili,madhara na tiba yake)


Tatizo la kuwashwa macho ni tatizo ambalo huwapata watu wengi na kuleta kero kubwa kama vile kupikicha macho kila dakika, macho kutoa machozi yenyewe N.K.


CHANZO CHA TATIZO LA KUWASHWA MACHO


Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia mtu kuwashwa na macho,na miongoni mwa sababu hizo ni kama vile;


- Kuwa na allegy ya baadhi ya vitu kama vile, Maji ya kisima,maji ya mvua, Sabuni,mafuta, N.K


- Dalili za macho kushambuliwa na baadhi ya magonjwa  mbali mbali ya macho


- Macho kuingiwa na dawa,perfume au kitu chochote chenye baadhi ya  kemikali 


- Baadhi ya watu huwashwa sana na macho baada ya kuingiwa na kitunguu, hali ambayo huweza kukaa kwa muda kidogo kabla ya kuisha yenyewe


- Jicho kuingiwa na vitu kama mchanga, pilipili N.K


DALILI ZA TATIZO LA KUWASHWA MACHO


- Kuhisi hali ya kuchoma ndani ya jicho


- Macho au jicho kubadilika rangi na kuwa jekundu


- Macho kutoa matongo tongo yenyewe


- Macho kuanza kutoa machozi yenyewe


- Macho kuwasha


MADHARA YA TATIZO LA KUWASHWA MACHO


- Macho kubadilika rangi na kuwa mekundu


- Huathiri uwezo wa uono wa macho yako


- Macho kuvimba


- Macho kutoa matongo tongo yenyewe


- Macho kutoa machozi yenyewe


- Kero ya kupikicha na kukuna macho kila dakika


MATIBABU YA TATIZO LA KUWASHWA MACHO


- Tiba hutegemea chanzo cha tatizo hili, lakini kwa upande wa dawa zipo dawa mbali mbali ambazo huweza kutumika kutibu tatizo hili kabsa.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!