TATIZO LA KUZIBA MRIJA WA MACHOZI MACHONI

 AFYA YA MACHO

• • • • •

TATIZO LA KUZIBA MRIJA WA MACHOZI MACHONI


Tatizo hili hutokea sana kwa watoto wadogo na wengi wao hupona wenyewe bila hata kupewa dawa yoyote, lakini ikitokea kwa mtu mzima huwa na shida kidogo kupona.


Na shida hii huweza kuhusishwa na sababu mbali mbali kama vile; 


✓ Mtu kuumia jichoni


✓ maambukizi ya bacteria au magonjwa mengine ya macho


✓ Mtoto kuzaliwa wakati tayari tatizo lipo ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Congenital blocked tear duct


✓ Mtu kuwa mzee sana


✓  dalili za kansa,uvimbe N.K


✓ Matumizi ya dawa za macho aina ya matone kwa muda mrefu


DALILI ZA TATIZO LA KUZIBA MRIJA WA MACHOZI MACHONI


- Mtu kutokuona vizuri au kuona marue rue

- Jicho kutoa sana machozi muda wote

- Sehemu nyeupe ya jicho kubadilika rangi na kuwa nyekundu

- Mtu kupata maumivu makali jichoni

- Jicho kuvimba 
N.K


MATIBABU YA TATIZO LA KUZIBA MRIJA WA MACHOZI MACHONI


• Zipo njia mbali mbali za kutibu tatizo hili kama vile; matumizi ya baadhi ya dawa za kuzibua mirija hii, mgonjwa kufanyiwa procedure ya Catheter eye dillation, Jicho kuflashiwa pamoja na Njia ya Upasuaji.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!