TATIZO LA MAJIPU(ugonjwa wa jipu)

 MAJIPU

• • • • •

TATIZO LA MAJIPU(ugonjwa wa jipu)


Ulishawahi kukutana na kauli kama hizi, kwamba ukiwa na majipu damu yako ni chafu? au una mchafuko wa damu mwilini? Soma hapa kujua zaidi..!!!


Tatizo la majipu kwenye maeneo mbali mbali ya mwili huhusisha mkusanyiko wa usaha kwenye upele au sehemu ya ngozi na huweza kusababishwa na vimelea mbali mbali vya magonjwa ikiwa ni pamoja na Bacteria jamii ya Staphylococcus aureus.


DALILI ZA TATIZO LA MAJIPU NI PAMOJA NA;


• Kupata kitu kigumu kwenye ngozi ukikishika ambacho huambatana na maumivu makali


• Kuona kitu kama kijiupele kikubwa kilichokusanya usaha ndani yake


• Ngozi ya eneo lililoathiriwa kuanza kubadilika rangi na kuwa nyekundu


• Mgonjwa kupandisha joto la mwili au mgonjwa kuwa na homa


• Wakati mwingine mgonjwa hupata miwasho sana sehemu ambapo kipele cha jibu kimetokea

N.K


MATIBABU YA TATIZO LA MAJIPU


- Zipo dawa mbali mbali ambazo huweza kutumika kumsaidia mtu kwenye shida ya majipu na miongoni mwa dawa hizo ni pamoja na matumizi ya Amoxicilin,  Ampiclox N.k


Kumbuka kuna aina mbali mbali za majipu na kila aina inatiba yake, Hivo ni vizuri kuongea na wataalam wa afya kwanza,kabla ya  kuanza matibabu yoyote.


-

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!