TATIZO LA MAUMIVU MAKALI YA KICHWA BAADA YA KULA KITU CHA BARIDI(ice cream headaches)
KICHWA
• • • • •
TATIZO LA MAUMIVU MAKALI YA KICHWA BAADA YA KULA KITU CHA BARIDI(ice cream headaches)
Tatizo hili la maumivu makali ya kichwa huanza baada ya mtu kula kitu cha baridi ambapo tatizo hili kwa kitaalam hujulikana kama Ice cream headache.
CHANZO CHA TATIZO HILI
-Maumivu haya ya kichwa hutokana na kichwa kupoozeshwa kwa gafla baada ya mtu kula vitu vya baridi kama barafu hali ambayo hupelekea mishipa ya kichwa kuvuta pamoja na kichwa kuuma.
DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;
- kuanza kupata maumivu makali ya kichwa baada ya kula kitu chochote cha baridi
- maumivu makali ya kichwa kwa mbele
- maumivu ya kichwa ambayo huweza kudumu kwa muda wa sekunde 20-60
- maumivu ya kichwa ambayo kwa mara chache sana huweza kufika dakika tano.
MATIBABU YA TATIZO HILI
Hakuna matibabu yoyote ya tatizo hili na wala huhitaji dawa yoyote kwani maumivu haya huisha yenyewe ndani ya muda mfupi, japo endapo maumivu yataendelea kwa zaidi ya masaa sita basi hilo ni tatizo lingine waone wataalam wa afya.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!