UZAZI
• • • •
TATIZO LA MOLAR PREGNANCY(chanzo,dalili na tiba)
Molar pregnancy ni hali ya ukuaji wa seli(trophoblasts) usio wakawaida ndani ya mfuko wa uzazi na kumfanya mwanamke kuonekana mjamzito na kuwa na dalili zote za mimba wakati hana mimba.
CHANZO CHA TATIZO LA MOLAR PREGNANCY
Tatizo hili la molar pregnancy hutokana na hitilafu katika urutubishaji wa yai ambapo hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo imeonekana kusababisha shida hii, japo kuna baadhi ya sababu ambazo huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata shida hii kama vile;
- Mwanamke kujaribu kubeba mimba akiwa na umri mkubwa mfano zaidi ya miaka 35
- Mwanamke kujaribu kubeba mimba kwenye umri mdogo sana mfani chini ya miaka 18
- Kuwa na shida hii kwa hapo kabla
- Matumizi ya baadhi ya dawa hasa ambazo huhusu kuongeza au kupunguza vichocheo mwilini
- Molar pregnancy haiwezi kuendelea na kukua kama mimba ya kawaida hivo mwanamke mwenye shida hii anatakiwa kwenda hospital kwa ajili ya vipimo zaidi na msaada wa kimatibabu
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!