TATIZO LA MOYO KWENDA MBIO(chanzo chake)

   MOYO

• • • • •

TATIZO LA MOYO KWENDA MBIO(chanzo chake)


Wakati mapigo ya moyo yanaenda kawaida,mtu hata anaweza asikumbuke kwamba kuna moyo ndani ya mwili wake unadunda siku zote, ila pale mapigo ya moyo yanapobadilika mfano; kwenda mbio sana, Mtu huanza kuhisi hali ya tofauti na kusikia sana moyo ukidunda.


Mapigo ya moyo kwenda mbio inaweza kuwa tatizo lakini pia inaweza kuwa ni hali ya kawaida kulingana na chanzo chake. Hivo katika makala hii tunaangalia sababu ambazo huweza kuchangia mapigo ya moyo kwenda mbio


SABABU ZA MAPIGO YA MOYO KWENDA MBIO NI PAMOJA NA;


- Baada ya mtu kufanya mazoezi mbali mbali ya mwili kama vile; kukimbia, kuruka kamba, kucheza mpira N.K


- Mabadiliko ya mwili ambayo hutokana na mabadiliko ya vichocheo mwilini kipindi cha ujauzito, wakina mama wengi wajawazito hupatwa na hii hali ya mapigo ya moyo kuongezeka au kwenda mbio


- Mtu kuwa na furaha sana iliyopitiliza huweza kusababisha mpaka mapigo yake ya moyo kubadilika na kwenda mbio


- Mtu kuingiwa na hofu kubwa pamoja na wasi wasi wa gafla kutokana na vitu mbali mbali mfano; baada ya kupokea au kusikia taarifa mbaya ya kifo cha mtu wake wa karibu N.K


- Matumizi ya vinywaji mbali mbali kama vile kahawa huweza kusababisha mapigo ya moyo kwenda mbio


- Uvutaji wa sigara zenye vichocheo vya Nicotin ndani yake


KUMBUKA; mapigo ya moyo kwenda mbio huweza kuwa ugonjwa au tatizo pale ambapo huambatana na shida nyingine na ikiwa ni hali ambayo huchukua muda mrefu na ya kutokea mara kwa mara



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!